Kiungo wa Chelsea Juan Mata amesajiliwa na
klabu ya Man Utd kwa dau la paundi mil 37. Mata anatarajiwa kufanya
vipimo kabla ya kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu hiyo. Taarifa
kutoka DailyMail zinasema kocha wa
Chelsea Jose Mourinho ameshasaini makataba wa kumuuza mchezaji huyu
kwenda Man Utd licha ya kuwa mashabiki wa Chelsea hawajapendezwa na
kuuzwa kwa mchezaji huyu. Mata anatarajia kutambulishwa wikiendi hii
na ataweza kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na United dhidi ya
Cardiff City siku ya jumanne.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment