Pwani ya kenya yashambuliwa. 48 wamekufa

Takriban watu 48 wameuawa baada ya watu
wanaoshukiwa wapiganaji wa kiisilamu
kushambulia hoteli na kituo cha polisi katika mji
wa Mpeketeni Pwani ya Kenya
Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema
makabiliano ya risasi yaliendelea kwa saa kadhaa
na kushuhudia majengo yakiteketezwa.
Mji wa Mpeketeni uko karibu na kisiwa cha Lamu ,
eneo linalosifika kama kivutio cha watalii
Kenya imekumbwa na mashambulizi tangu mwaka
2011 ilipopeleka wanajeshi wake nchini Somalia
kupambana na wapiganaji wa Al Shabaab
Mashambulizi yanaarifiwa kuanza saa mbili usiku
wenyeji walipokuwa wanatazama michuano ya
kombe la dunia
Wakazi waliambia BBC kuwa watu waliokuwa
wamejihami walivamia gari moja ambalo
walilitumia kufanyia mashambulizi katika maeneo
tofauti ya Mpeketoni
Wakazi wanasema washambuliaji walikuwa
wamejifunika nyuso zao na kisha kutupa
maguruneti katika kituo cha polisi kabla ya kuingia
na kuiba silaha

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment